google.com, pub-4324601895065941, DIRECT, f08c47fec0942fa0

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MASHETANI WALIOKATAZA WATU MEMA WAPINDULIWAPINDULIWA NA MWANAMAPINDUZI.


IBADA YA JUMAPILI YA TAREHE 02_11_2014

MCHUNGAJI  MAXIMILLIAN  MACHUMU

SOMO: ALIKATAZWA MEMA NA MASHETANI


Mchungaji maxmilian Machumu
“Wakafika ng'ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi.  Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu;  makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo;  kwa
Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima
sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda.  Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikata-kata kwa mawe.  Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia;  akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese.  Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi.  Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile.  Na hapo milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, wakilisha.  Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao.  Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini.  Wachungaji wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka walione lililotokea.  Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa.  Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na habari za nguruwe.  Wakaanza kumsihi aondoke mipakani mwao.  Naye alipokuwa akipanda chomboni, yule aliyekuwa na pepo akamsihi kwamba awe pamoja naye;  lakini hakumruhusu, bali alimwambia, Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawahubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu.  Akaenda zake, akaanza kuhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakastaajabu.” Marko5: 1 - 20

Mema ni fungu la wana wa Mungu, lakini linayo gharama ya kulipia ambayo ni utii. Kuna watu leo wamekataliwa kutenda na kupokea mema na shetani kwa kukosa utii.

Mgerasi huyu anayeongelewa katika kitabu cha Marko alikataliwa mema kwa kuwahiwa kwenye akili yake. Akashidwa kuwaza mambo mema. Akili ilipofungwa hakuwaza mema na kwasababu hakuwaza mema hakutenda mambo mema na kwasababu hakutenda mema hakupata mema pia. Akawa na mazoea ya kutenda na mwisho hatma yake haikuwa njema. Tatizo la watu wengi ni mawazo yao. Unapowaza mawazo mazuri utatenda mambo mema na mema yanakufuata. Waweza kuwa milionea leo lakini kama una mawazo ya kimaskini ni muda tu kabla hujawa maskini.

Huyu mgerasi aliwaza na miguu yake ikampeleka mpaka makaburini na midomo yake ikaanza kupiga kelele na mikono ikaanza kujikata. Ni kwasababu ya mawazo ya mashetani yaliyoingia ndani yake yalimpeleka makaburini mbali na makusudi ambayo Mungu aliyaweka ndani yake. Kumbe kuna mawazo ambayo mtu huwaza na ni ya kishetani na yana lengo la kumpeleka mbali na makusudi ya Mungu katika maisha yake.

Watu wengi leo wanaishi matokeo ya mawazo waliyowaza ambayo yalikuwa ya kishetani na ndio yaliyowapelekea kupatwa na uchungu bila ya wao kujua. Unapoanza kuwaza mambo yasiyo ya kawaida jua kwamba shetani anatafuta kitu ndani yako au anajaribu kupindisha kusudi la Mungu katika maisha yako.

Kuna mawazo mengine yanakuja ndani ya watu yanaonekana kana kwamba ni ya  ki-Mungu lakini ni ya kishetani.  Baadae mawazo haya huharibu mema ambayo Mungu alipanga kwa ajili ya maisha ya mtu huyu. Na kawaida shetani akishakupa wazo moja baya na wewe ukalipokea, shida itakapokupata atakupa wazo la pili na la tatu mpaka ahakikishe amekutoa nje kabisa ya kusudi la Mungu. Kuna mawazo Mungu ameshatuwekea ndani yetu ili tuwe watu wema na wenye kuzaa mema. Lakini shetani kwa kulitambua hili huwahi ndani ya akili zetu  na kupandikiza mawazo ya ubaya.  Hivyo maisha ya mtu huyu yanakuwa yameandamwa na kila baya; misiba, kushindwa, kukataliwa.

Na ili usije ukahangaika na kupata akili zako tena, shetani huweka walinzi ili wahakikishe hurudi kwenye kusudi la Mungu. Walinzi hawa ndio majini, mizimu na miungu mbalimbali. Mfano yawezekana kuna mtu ambaye ukishirikiane naye katika biashara utafanikiwa kwa sababu ipo baraka ya kiMungu kwa ajili yako ndani yake; walinzi hawa huhakikisha wanakupindisha uende kwa mtu tofauti atakaye kupeleka katika laana.

Lakini ninayo habari njema kwako leo; ya kwamba hata shetani na mawakala wake wakupeleke mbali kiasi gani na kusudi la Mungu yupo mwanaume Yesu atakufuata huko huko. Kama alivyomfuata yule mgerasi kule makaburini na wewe pia atakufuata. Simama leo, chukua nafasi yako kama mwana wa Mungu ukatii ili upate kula mema ya nchi.

 

 UKIRI

Kwa mamlaka ya Jina la Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai ninawashia moto mashetani wote mnaoniletea mawazo mabaya kwenye akili yangu, mnaopindisha mawazo yangu ambayo Mungu ameniwekea kwa jina la Yesu. Ninawasha moto kwa mashetani yote yanayonijia kupindisha njia zangu kwa damu ya mwana kondoo, kuanzia leo mimi sio maskini kwa jina la Yesu. Imeandikwa; “mwana wa Mungu alidhihiriswa ili azivunjee kazi za ibilisi kuzimu,” Ninazivunjavunja kazi zote za kuzimu kwa jina la Yesu kristo, mnaopindisha mawazo ya maendeleo yangu ninawafyeka kwa upanga wa Kristo. Katika jina la Yesu enyi jeshi la mashetani mliotumwa kuja kuniletea matatizo kwenye maisha yangu ninawatetekeza kwa moto wa Mungu. Imeandikwa, “neno la Mungu ni moto ulao.” Ninawateketeza mashetani wote mliotumwa na waganga wa kienyeji, wachawi mmetokea kuzimu ninawateketeza kwa moto wa Mungu kwa jina la Yesu.

Asante Bwana Yesu kwa kunifuata na kuniokoa leo, nipe neema ya kuishi sawasawa na mapenzi yako ili niweze kupokea yale mema ambayo ni haki yangu kama mwana wa Mungu. Amina!

 


 

 

 

 





 

 

 

Post a Comment

0 Comments